A

A

TAARIFA YA KATIBU WA BUNGE MAALUM KWA VYOMBO VYA HABARI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
nembo-taifa.gif.pagespeed.ce.PYaHE5b175
BUNGE MAALUM 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM TAREHE 17 HADI 21 MACHI, 2014 
Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dodoma kesho kwa ratiba ifuatayo:
Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa.
Hivyo Wajumbe wote ambao hawajaapa kiapo cha ujumbe wa Bunge Maalum wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum kesho saa 2:00  asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.
Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum.
Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za Bunge Maalum.
Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania.
Tarehe 21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Bunge Maalum na saa 10:00 jioni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa Bunge Maalum 
Atakaye ipata taarifa hii amjulishe mwenzake. 
Imetolewa na Ofisi ya
KATIBU WA BUNGE MAALUM