Klabu ya Simba, imetajwa kuwa mpango wa kumrejesha
mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Haruna Moshi ‘Boban’ kwa ajili ya
msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Bobab aliyetemwa katika msimu uliopita na
kwenda Coastal Union ya
Tanga, Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, iliyo chini ya Mwenyekiti wake,
Zacharia Hanspope iko mbioni kumrejesha kwa ajili ya kuichezea tena timu
hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi,
Mtu wa karibu aliupasha mtandao huu kuwa Boban atarejea tena Simba kwa ajili ya kuendelea kuitumikia msimu ujao.
Ilielezwa wameona umuhimu wa kumrejesha Boban ili kujenga kikosi
kipya baada ya kujiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa wa
ligi hiyo.
“Sisi hatupo katika mbio za ubingwa, tulichoamua kwa sasa ni kuijenga
timu yetu ili msimu ujao tuweze kufanya vizuri,”alisema kwa masharti ya
kutajwa jina lake kwa kuwa sio msemaji wa klabu.
Msemaji wa Simba, Asha Mhaji, alisema kuwa huo si wakati wake kujadili usajili wao kwakuwa ligi bado haijamalizika.