SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa linasubiri barua toka serikali
ili kujua gharama za mlango wa kioo uliovunjwa na kiungo wa Simba
Ramadhani Singano ‘Messi’.
Jumapili
iliyopita kiungo huyo wa Simba alifanya uharibifu ndani ya Uwanja wa
Taifa katika vyumba vya
kubadilishia nguo ‘dressing rooms’ kwa kupiga
teke mlango na kusababisha kuvunja vioo vya mlango huo.Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura, alisema wanasubiri tamko kutoka kwa serikalini ndipo watajua adhabu ya kumchukulia staa huyo.
Wambura alisema baada ya kupata gharama hizo TFF italipa lakini
baadaye wataipiga faini Simba.“Bado hatujajua gharama ni shilingi ngapi,
tunasubiri serikali watuambie na baada ya hapo sisi tutalipa na
kuwaandikia barua Simba ili waturudishie fedha zetu,” alisema Wambura.
Wakati Wambura akisema hivyo, Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake
Asha Muhaji imesema kuwa inasubiri TFF iwaambie kiasi cha fedha
wanachodaiwa ili nao waweze kumkata mchezaji huyo.
“Tunasubiri tamko la TFF, tukifishafahamu hilo ndipo tutajua ni kitu
gani cha kufanya baada ya kutoa hilo tamko na kwa upande wetu, huenda
Messi akachukuliwa hatua vilevile ili kuweza kudhibiti nidhamu kwa
wachezaji wetu,”alisema Muhaji