Macho na
masikio yote Jumamosi ya leo yataelekezwa Lagos ambako tuzo za AMVCA (Africa
Magic Viewr's Choice Awards) zitafanyika. Tuzo za AMVCA zilianzishwa ili
kutambua na kusherehekea mchango wa wandaaji filamu, waigizaji na wataalam wa
Afrika kufuatia mafanikio ya Bara hili katika tasnia ya filamu na televisheni.
Tanzania
inajivunia kuwa sehemu ya mashuhuda, kufuatia kupendekezwa katika vipengele
kadhaa kutoka tamthilia maarufu, Siri ya Mtungi iliyoingia katika vipengele
vifuatavyo:
·
Best Make Up – Rehema Samo
·
Best Wardrobe – Doreen Estazia Noni
·
Best Art Direction – Kyle Quint
·
Best Sound Editor – Jordan Riber
·
Best Actor in a Drama – Juma Rajab
·
Best Indigenous language movie/series – Jordan Riber
·
Best TV Series (comedy/drama) – John Riber
Timu nzima
itakayoondoka itasindikizwa na Waziri wa Habari, Dr. Fenella Mukangara.
Tuzo za mwaka jana
zilihudhuriwa na baadhi ya majina makubwa katika uigizaji barani Afrika. Baadhi
ya filamu ambazo zilibeba tuzo zilikuwa Otelo Burning (Filamu bora), Skeem
(Filamu bora - Ucheshi) na The Mirror Boy (Filamu Bora ya tamthlia). Waigizaji
Bora wa kike na kiume walikuwa OC Ukeje toka Nigeria na Jackie Appiah wa Ghana.
Watazamaji
wanaweza kuangalia tukio zima la utoaji wa tuzo kupitia Africa Magic kuanzia
saa moja jioni.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako