Siku
zinahesabika toka Wasanii watatu wa bongofleva ambao ni Snura, Jux na
Dully Sykes kutangaza kwamba video zao za ‘nimevurugwa, uzuri wako na
kabinti special’ zimepigwa stop kuonyeshwa kwenye TV za Tanzania
kutokana na kuvuka mipaka ya kimaadili japo bodi ya filamu Tanzania
imekanusha.
Mwenye huu wimbo hapa ni Mkenya, anaitwa Blaqy ambae pamoja na
video
yake kupigwa marufuku kuonyeshwa kwenye TV nchini Kenya, kwa mujibu wa
mitandao mbalimbali bado aliendelea kushikilia msimamo wake kwamba video
hiyo haikua na tatizo lolote.
Alikaririwa kwenye barua aliyoiandika kwa bodi ya filamu Kenya kutaka
kuifungulia hii video na kuacha kuzembea nafasi iliyopo kwa vijana
kujitengenezea ajira nyingi kwenye kiwanda cha muziki.
Vyombo mbalimbali vya habari viliripoti kwamba Blaqy alisema hata
hivyo huu wimbo haukupata nafasi kwenye media kwa sababu Watangazaji na
Dj’s wameendekeza rushwa ya ngono na pesa.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako