Mmoja wa washiriki katika mbio za Vaisakhi rally 2014 akionesha umahiri wa kupita vikwazo katika njia iliyotumika kwa ajili ya mashindano hayo. |
Team Viduku wakitafakari baada ya gari lao la mashindano kupata hitilafu wakati wakiwa katika mzunguko wa pili wa mashindano ya Vaisakhi rally 2014. |
Wananchi wa mjini Moshi, waliojitokeza kushangilia magari katika eneo la Mabogini katika mbio za mwaka huu za magari za Vaisakhi |
Moja ya magari yaliyoshiriki mashindano ya mwaka huu ya Vaisakhi Rally, yaliyofanyika jana mjini Moshi. |
Gari aina ya Mitsubishi linaloendeshwa na Dereva mkongwe, Gerrad Miller likikatiza kona katika eneo la Newland. |
Gurjit Dhani akichana mbuga katika eneo la Newland. |
Gurjit Dhani |
Gari namba 32, linaloendeshwa na Dereva Amarjeet Dhillon wa Arusha akichanja mbuga katika mashindano ya mwaka huu ya Vaisakhi Rally. |
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Vaisakhi Rally mwaka huu, Gurjit Dhani (kushoto) na Msaidizi wake Shameer Yusuf wakishangilia ubingwa wao. katikati ni Afisa michezo wa mkoa wa Kilimanjaro, Anthony Ishumi. |
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Vaisakhi Rally mwaka huu, Gurjit Dhani (kushoto) akimpa zawadi ya ushindi Baba yake Mzazi, Mzee Dhani wa Charang Singh, Kulia ni Msaidizi wake Shameer Yusuf. |
Washindi wa nafasi ya tatu hadi ya kwanza katika mashindano ya mwaka huu ya Vaisakhi Rally. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. |