A

A

NISHA ANANGWA KUMWANIKA MTOTO MWENYE UKIMWI

           Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ akiwa na mtoto aliyemwanika laivu mitandaoni.
Stori: Mwandishi Wetu
OOHOOO! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amenangwa kutokana na kitendo chake cha kumwanika laivu mtoto anayeishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).
Nisha akiwa kwenye baiskeli na mtoto huyo anayeishi na Virusi vya Ukimwi (VVU)..
Hayo yalijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mwigizaji huyo alikwenda visiwani Zanzibar kumsaidia mtoto huyo asiye na wazazi ambaye amekuwa akitengwa na watoto wenzake shuleni na mitaani kutokana na kuishi na virusi hivyo.

Kupitia mitandao ya kijamii, Nisha alitundika picha ya mtoto huyo bila kumziba sura kisha akaandika: “Huyu mtoto ndiyo sababu hasa iliyonifanya nikaja huku, yupo darasa la pili, ana miaka 9, baba yake alimkana akiwa tumboni mwa mama yake, ambaye alifariki pindi tu alipomzaa.
...Akiwa amembeba mtoto huyo.
“Mtoto huyu mdogo anaishi na Virusi vya Ukimwi, jamii inayomzunguka imemtenga, wazazi hawataki watoto wao wacheze naye, shule mwanzo alikataliwa, kula yake Allah anajua, yupo mpweke, SISEMI HIVI KUMTANGAZA LA HASHA ila ikumbukwe mimi ni msanii na ni kioo cha jamii.
“Jamii inatakiwa ione na kujifunza, inauma sana, ila nipo hapa kwa ajili yake.”
Baada ya hapo, kuna baadhi ya mashabiki wake walimpongeza kwa kuonesha mfano wa kusaidia jamii hasa watoto lakini upo upande wa pili uliomnanga kwa kutojua kuwa kumwanika mtoto wa aina hiyo kunaweza kumwongezea unyanyapaa.
“Ni kweli inauma na Nisha umefanya jambo jema kumsaidia lakini kwa kumwanika hadharani mimi siungi mkono ni bora hata ungemziba. Huku ni kumuongezea unyanyapaa,” aliandika mtoa maoni mmoja.
Mwingine akaandika: “Acha hizo wewe Nisha.
Mbona watu kibao wanasaidia bila kukiuka maadili na haki za binadamu? Kweli kwa upande huo haijatulia.”
Nisha alikwenda visiwani humo katika Kijiji cha Donge, Unguja ambapo alisaidia familia saba ambazo hazina msaada, hata hivyo kitendo cha kumwanika mtoto huyo kilitia doa misaada aliyoitoa ingawa wapo waliosema kuwa inawezekana alifanya m