Karibu
kwenye kalamu au KKK ni jina la single mpya ya Roma Mkatoliki ambayo
ina wiki kadhaa tu tangu itoke ambapo leo imeingia kwenye headline baada
ya Roma ku-amplify mbele ya kipaza sauti cha millard kuhusu KKK.
Kama
umeisikiliza KKK ni wimbo ambao kidogo una maneno makali pengine ambayo
kwa sababu za kimaadili walizizima izo sehemu sasa kuna taarifa ilitoka
kuwa mara baada ya mama yake mzazi kuusikia wimbo huo alimnunia kwa
siku 4.
Roma ameanza kwa kusema>>’Kweli mwanangu mama alivosikiaga KKK
alichukia sana na kuniuliza kwanini nimetukana kwenye wimbo,basi baada
ya hapo kila nikimpigia akawa hapokei simu zangu karibu siku 4′.
Roma pia amesema kuwa KKK ndiyo single yake ambayo mpaka sasa
inamshangaza kwa aina ya matukio yanayojitokeza ikiwemo ile ya madereva
boda boda na Bajaj kuandamana hadi studio ilikotengezwa huo wimbo kuomba
kuwekewa kwenye flash na memory card zao kwa ajili ya kusikiliza.