Jokate Mwegelo amechukua nafasi ya Vanessa Mdee kama mtangazaji wa show
mpya ya kituo cha TV1 kilichozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Awali
Vanessa ndiye aliyekuwa amechukuliwa kuendesha kipindi hicho na tayari
alikuwa ameanza kurekodi vipindi. Haijulikani mabadiliko hayo
yamesababishwa na nini.
Jokate Mwegelo atakuwa akiendesha kipindi hicho akishirikiana na
mtangazaji wa zamani wa Kiss FM na Times FM, Ezden Jumanne aka The
Rocker.
Ezden Jumanne akiongea na waandishi wa habari leo kwenye uzinduzi wa kituo hicho uliofanyika jijini Dar. Pembeni yake ni Jokate Mwegelo
Jokate Mwegelo akiongea na waandishi wa habari
Show hiyo ni version ya Tanzania ya show kama hiyo inayorushwa kwenye
kituo cha TV cha Viasat cha Ghana ambacho nacho kinamilikiwa na kampuni
moja inayoimiliki TV1, MTG ya nchini Sweden.
Picha: Othman Michuzi
Picha: Othman Michuzi