Suala la msanii wa Kenya, Colonel Mustapha kupost picha akiwa na
Huddah Monroe zilizoweka alama nyingi za kuuliza kwa wana maadili
limeendelea kuwa mwimba kwake.
Siku kadhaa baada ya Huddah kudai kuwa hawana uhusiano wowote na
Mutapha zaidi ya kupiga picha ili kumpa kick msanii huyo, wanawake wa
Pwani wakiongozwa na mwimbaji wa kike wa Kenya Nyota Ndogo waliandamana
wakilaani vitendo vya Colonel kwa madai kuwa amewadhalilisha wanawake.
Wanawake hao walikuwa na mabango yaliyoondikwa “Colonel Mustapha
heshimu wanawake, Mustapha Komesha dhuluma kupitia mtandao heshimu
muziki, Wanawake ni dada zako na mama zako,” na mengine.
Mustapha ameguswa na maandamano hayo na ameomba msamaha wakati anaongea na mtangazaji maarufu Mzazi Willy M. Tuva.
“Ninawaomba msamaha kwa sababu ni lazima tu-respect wamama.”