MSANII
kutoka jiji la Mwanza ambaye alipata umaarufu kupitia Shindano la BSS
amevunja ukimya na kusema mambo mengi juu ya Msanii wa Filamu ambaye
wanatoka wote jiji moja la Mwanza ambaye anajulikana kwa jina la Suzane
Michael. Kala alifunguka hayo na kusema kuwa "Nawashangaa sana hawa
madada zetu yani wao wanaona kujiachia ndiyo wataishi mjini, huyu dada
mimi namfanhamu na sikutegemea kama ataweza kupiga picha za hivi na
kuziweka mtandaoni yani kwa hiki kitendo ameuvuruga moyo wangu na
kuuchafua kabisaaaa" alisema Kala
Mwanadada
Suzane Michael
Hata ivyo kala alizidi kuongeza "Unajua kule kwetu Mwanza mtoto wa kike
anajiheshimu sana na ndiyo maana wanazidi kupendeza ila wakija Dar tu
kila kitu kinakuwa nyuma mbele mbele nyuma." aliongezea,