Jarida
la Washington Post nchini Marekani limeripoti kwamba askari watatu
wameachishwa kazi kwa muda na kurudishwa nyumbani ili uchunguzi
ufanyike.
Askari mmoja kati ya hao ambao wanaohusika na kumlinda rais Barack
Obama alikutwa amelewa pombe chakari kwenye hoteli moja huko Amsterdam
ambapo Obama alienda huko kwa ajili ya mkutano wa mambo ya Nuclear.
Msemaji wa idara ya upelelezi Marekani alikataa kutoa taarifa zaidi
kuhusu tukio hilo ingawa alisisitiza kuwa watatu hao wameachishwa kazi
kwa muda uchunguzi ukiendelea.
Mwaka 2013 majasusi wawili waliondolewa katika kikosi cha ulinzi cha
Rais Obama kufuatia tuhuma za kuhusika na kashfa ya ngono na utovu wa
nidhamu.
Mwaka 2012 majasusi kadhaa waliachishwa kazi kufuatia madai kuwa walikodi makahaba walipokuwa mjini Cartagena Colombia.