A

A

Mengine Kuhusu Marehemu Magwair na Hii Project Mpya Kwaajili Yake

Producer mwenye vipaji vingi,Mswaki ambaye pia ni mmiliki wa studio ya Black Curtains Records, ana project inaitwa Keeping Ngwair Alive, itakua ni album yenye ngoma kadhaa, Mswaki pia ana rap kwa kutumia style ya Albert Mangwea.Imefahamika kuwa marehemu albert mangwea aliwahi
kumkataza producer mswaki kutumia style yake.
Tayari Mswaki ameshaachia ngoma mbili mojawapo ni Open Later na nyingine inaitwa Ghetto ambayo ameachia hivi karibuni,Clouds fm ilimuuliza mswaki, je kama Ngwea angekua hai angerap kwa style hiyo?Mswaki pia amezungumzia mpango wake wa kwenda kupata baraka za mama albert, kabla ya kuifanya project hiyo kwa ukubwa zaidi ambapo anatarajia kuondoka kesho kuelekea Mkoani Morogoro kuongea na familia ya Mangwea. Swali je, Mswaki atakubaliwa kufanya anachokifanya kutoka kwa familia ya Albert Mangwea?