A

A

Kwa Mashabaiki wa Mbeya City,Hii ndio Taarifa Kutoka kwenye Timu yenu

Naomba kuwajulisha kuwa timu yetu imeondoka rasmi Mbeya leo tarehe 19/3/2014 kuelekea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Ruvu JKT mchezo huo utachezwa tarehe 22/3/2014 katika uwanja wa Azam Complex, chamazi.
Kwa ujumla wachezaji wetu wote wapo katika hali nzuri tayari kwa
mchezo huo isipokuwa mchezaji Richard Peter ataukosa mchezo huo maana hali yake haijatengemaa baada ya kuumia katika mechi yetu dhidi ya Rihno Rangers ya Tabora mchezaji huyu ana maumivu ya kawaida katika mbavu zake
Maandalizi yetu ni mazuri sana tumejiandaa vizuri tupo kamili kuzinyakua pointi tatu hii ni kwa mujibu wa kocha mwambusi anasema kikosi chake kina uwezo mkubwa sana wa kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Kwa niaba ya club natumia nafasi hii kuweka wazi kuwa tutakuwa makini sana na mchezo huu maana tumekuwa tukionyeshwa michezo mibaya sana na hasa kwa hizi timu za majeshi tunapokutana nazo mfano mzuri ni mchezo wetu dhidi ya Rihno Rangers wachezaji wetu waliumizwa kwa makusudi kabisa pia tutakuwa makini zaidi na maamuzi ya referee tunaomba mwamuzi atakae chezesha mchezo huo kuzingatia kanuni na sheria uwanjani ili kutoa haki kwa pande zote mbili.
Nawaomba mashabiki wetu waendelee kutuamini maana bado tunayo nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.
FREDDY JACKSON
AFISA HABARI
MCC FC
0757711486