Mwenyekiti
wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akiongoza kikao cha kwanza cha kamati
ya Uongozi baada ya kuundwa leo. Kamati hiyo inayoundwa na wenyeviti wa
Kamati za Bunge Maalum wote 12 pamoja na mambo mengine inajukumu la
kaundaa ratiba ya Bunge Maalum. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge Maalum
Yahya Khamis Hamad na aliyekaa kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge
Maalum Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Naibu
Katibu wa Bunge Maalum Dkt. Thomas Kashililah akitoa ufafanuzi kwa
wajumbe wa kamati ya Bunge Maalum kuhusu uwezo wa kutumika kupigia kura
vifaa vya kielekroniki vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge wakati
kamati hiyo ilipokutana jana.
Mjumbe wa Kamati ya Uongozi Mhe. Anna Abdalah akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe...Picha na Owen Mwandumbya
Na Magreth Kinabo, MaelezoDodoma
Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Samwel Sitta leo, ametangaza majina ya
wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za bunge hilo.
Majina hayo yametangazwa na Mwenyekiti huyo baada ya uchaguzi wa viiongozi hao uliofanyika (jana) Machi 24 , mwaka 2014 mjini Dodoma .
Mwenyekiti
huyo aliyataja majina hayo katika Kamati ya Uandishi
Mwenyekiti Andrew Chenge, Makamu wake ni Mgeni Hassan Juma. Kamati ya
Kanuni Mwenyekiti ni Pandu Ameri Kificho, Makamu wake ni Dkt. Susan
Kolimba. Kamati Na. 1 Mwenyekiti ni Ummy Ally Mwalimu, na Makamu wake
ni Prof. Makame Mbalawa.
Wengine waliochaguliwa katika Kamati Na. 2 Mwenyekiti ni Shamsi Vuai Nahodha, Makamu wake ni Shamsa Mwangunga.Kamati Na. 3 Mwenyekiti ni Dkt. Francis Michael, Makamu wake ni Fatma MussaJuma.
Mhe.
Sitta alisema waliochaguliwa katika Kamati Na. 4 Mwenyekiti
ni Christopher Ole-Sendeka, Makamu wake ni Dkt. Sira Ubwa Mamboya,
Kamati Na. 5 Mwenyekiti ni Hamad Rashid Mohamed Makamu wake ni Assumpter Mshama.
Viongozi waliochaguliwa katika Kamati Na. 6 Mwenyekiti Stephen Wassira na Makamu wake ni Dkt. Maua Daftari.Kamati Na. 7 Mwenyekiti Brig. Hassan Ngwilizi ,Makamu wake Waride BakariJabu.Kamati Na. 8 Mwenyekiti ni Job Ndugai,Makamu wake ni Biubwa Yahya Othman.
Kamati Na. 9 Mwenyekiti ni Kidawa Hamidi Saleh,Makamu wake Wiliam Ngeleja,Kamati Na. 10 Mwenyekiti ni Anna Abdallah, Makamu wake ni Salmin Awadh Salmin.Kamati Na. 11 Mwenyekiti ni Anne Malecela, Makamu wake Hamad Masauni na Kamati Na. 12 Mwenyekiti Paul Kimiti na Makamu wake ni Thuwaybah E. Kisasi.
Wakati huohuo , Sitta alitangaza wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba, ambao ni wenyekiti na makamu wenyeviti wa kamati hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua.
Wajumbe
hao walioteuliwa na Sitta kuingia katika kamati hiyo ni Fakharia
Khamisi Shomari, Mary Chatanda, Profesa Ibrahim Lipumba, Amon Mpanju na
Hamad Abuu Juma.
Hata hivyo pamoja na majina hayo kutangazwa Profesa Lipumba alisimama na katika nafasi hiyo .