A

A

Hii ni Serious Case Kwa Watanzania Wote Wanaotafuta Nyumba za Kupanga Jijini Dsm/Sinza

WADAU KUWENI MAKINI..... HEBU SOMA HII STORY
Nimetapeliwa Sinza
Ndugu zangu nisaidieni kama naweza kuwapata walionitapel na warejeshe malipo niliyoyatoa.

Siku moja nilienda Sinza kwa Remy nikitafuta nyumba!Nilionyeshwa dalali na nikazunguka naye,nyumba alizonionyesha sikuridhika nazo!Baada ya cku 2 nikapigiwa simu na akasema umepata nyumba?Nilimjibu bado then kanambia njoo kwa Remi kuna nyumba!Ndugu zangu nilitoka Posta Haraka,nilipofika Kwa remi nilimpigia simu akanambia kuwa yeye ameenda kumuonyesha MTU shamba lkn ana kijana wake anaitwa Fred,after 6mins alikuja kijana akatupeleka kuangalia nyumba.Niliona nyumba nikamuuliza mwenye nyumba yupo wapi?Akasema Makongo!Kesho yake huyu Fred(0656389300) akatupeleka makongo kwa Mwenye nyumba tukalipa.

Siku ilifika ya kuhamia kabla ya kuhama tuliwasiliana na yule mwenye nyumba hapatikan kwa simu.Kumbe tumelipa kwa MTU fake.Nilifungua RB na nilienda na police wawili pale nilipolipia geti halikufunguliwa!Siku nyingine niliwachukua ten a police wa upelelezi tukavizia mvua inanyesha tukapiga hon getin geti likafunguliwa na Kijana akatukaribisha sebulen,wale polisi wakiwa na nguo za kiraia walimuuliza yule kijana mzee yupo akasema yupo wakamwambia sisi nin wagen wake.Ile nyumba INA kigorofa na yule kijana alipanda juu dk5 akashuka akasema kwan hamkuwasiliana na Mzee kwa simu?

Mzee hayupo yupo Zanzibar na anakuja Leo jion,.Police walimwabia yule kijana Tupe namba zake yule kijana akatoa namba na polisi alipiga ile no. Jamaa akapokea akasema hayupo Zanzibar na anafanya kazi bank na hataki usumbufu kama police WAPO kwenye nyumba yake basi waichukue au waichome moto,Ila huyu jamaa naamin alikuwa ndan nikawambia polisi wakasema hawana search warrant.Tukarudi.

NDUGU ZANGU NAWAOMBENI MAWAZO YENU AU USHAURI ili tuwakamate hawa matapeli waweze kurudisha hizi hela kwan nilikopa ndugu zangu.W

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako