Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
TIMU
ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza imeondoka leo
(Machi 26 mwaka huu) kwenda Brazil kushiriki mashindano ya Kombe la
Dunia kwa Watoto wa Mitaani.
John
Kadutu ambaye ni mjumbe wa Bodi ya kituo hicho, na pia mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha
klabu za Mkoa wa Mwanza ndiye kiongozi wa msafara wa timu hiyo ya
Tanzania.
Michuano
hiyo ya siku 10 inayoshirikisha watoto wa mitaa (wavulana na wasichana)
inaanza keshokutwa (Machi 28 mwaka huu). Nchi 19 zinashiriki michuano
hiyo itakayofanyika katika Jiji la Rio de Janeiro.
Mbali ya Tanzania, nchi nyingine zinazoshiriki michuano hiyo kwa upande wa wavulana ni Argentina, Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe. Mwaka 2010 mashindano hayo yalifanyika Durban, Afrika Kusini ambapo pia Tanzania ilishiriki.