TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo imetoka sare ya
kufungana bao 1-1 na Namibia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki
uliochezwa kwenye uwanja wa Sam Nujoma nchini Namibia.
Dakika ya 30 ya kipindi cha pili Stars ilifanya mabadiliko kwa kutoka Erasto Nyoni na Juma Luizio na kuingia Michael Pius na Mcha Khamis
Ilipoingia dakika ya 85 Stars baada ya kuona mambo bado mazito wakafanya mabadiliko mengine akatoka Ramadhan Singano na kuingia Athanas Mdamu.
Taifa stars ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 86 kupitia kwa Khamisi Mcha 'Viali' kwa mpira wa kona aliopiga na kuingia moja kwa moja mpaka kwenye nyavu za Namibia bila kuguswa.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako