Juzi
tarehe 18/03/2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini
Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha kwenye Bunge maalum la Katiba
rasimu ya pili ya katiba.Toka
awasilishe rasimu ile bungeni , kumekuwa na maombi mengi sana ya kutaka
kujua kama msimamo wa CCM juu ya baadhi ya mambo hasa muundo wa
muungano bado ni uleule.Kwasababu
ya maombi hayo CCM imeona bora kueleza kwa mara nyingine tena msimamo
na imani ya CCM juu ya swala zima la Muungano na muundo wake.Kimsingi
CCM ndio waasisi wa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar. CCM
inamasilahi makubwa na mapana na Muungano huu kama waasisi pengine
kuliko taasisi nyingi ndani na nje ya nchi yetu.
Bado
CCM inaamini changamoto za Muungano huu suluhisho lake sio kubadili
muundo wa Muungano bali ni kuufanyia maboresho muundo wa muungano
tulionao wa serikali mbili. Hivyo basi CCM bado inaamini muundo bora
kwasasa utakao dumisha muungano wetu ni muundo wa SERIKALI MBILI.
Kwakuwa
kazi ya Warioba na Tume yake sasa imekwisha rasmi, kuisha kwa kazi yao
ni mwanzo wa awamu nyingine ya mchakato huu. Mwisho wa kazi ya Tume sio
mwisho wa mjadala juu ya Katiba tuitakayo bali ni mwanzo wa awamu
nyingine ya mjadala mpana na maboresho kama sio marekebisho ya kuondoa
mapungufu kwenye rasimu iliyowasilishwa.
Mwanzo
wa awamu hii nyingine ni furusa nzuri ya kupima kama kweli yaliyomo
kwenye rasimu na maelezo ya ziada yaliyotolewa na Jaji Warioba yana
akisi maoni ya Watanzania walio wengi.
CCM
ina amini awamu mbili zilizobaki kwakuwa zinahusisha wawakilishi wa
wananchi kupitia Bunge maalum la Katiba, na hatimaye itawahusisha
wananchi wenyewe moja kwa moja kupitia kura yao, zitatumika vizuri
kutupa ni nini hasa matakwa ya Watanzania juu ya Katiba waitakayo na sio
maoni au matakwa ya wachache.
Wakati haya yote yakiendelea CCM bado tunaamini Muungano huu ni muhimu ukadumishwa na kuimarishwa. CCM tunaaamini ili Muungano huu udumu njia pekee kwasasa ni kufanya marekebisho kwenye Muundo wa serikali mbili ili ujibu vizuri zaidi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na kukidhi mazingira ya sasa.
Tunawaomba wanaCCM na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu katika kipindi hiki. Ni vizuri Watanzania tukavumiliana,tukashindana kwa hoja tukitanguliza mbele uzalendo na masilahi ya kweli ya nchi yetu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
20/03/2014
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
20/03/2014
Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity
CCM Secretary for Ideology & Publicity