AMA kweli mchepuko ni balaa! Jamaa
aliyefahamika kwa jina moja la Peter amekiona cha moto baada ya kufanya
mchepuko na mke wa rafiki yake bila kufahamu kuwa kufanya hivyo ni
hatari kwa maisha yake, Risasi Jumamosi lina kisa na mkasa.
Kama kawaida, hivi karibuni, Mkuu wa
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, akiwa chumba cha
habari, alipokea simu kutoka kwa ‘kaka mkubwa’ mmoja aliyeomba hifadhi
ya jina na kueleza kuwa alimtilia shaka mke wa kaka yake na yupo njiani
na bodaboda akimfuatilia.
Shemeji mtu alidadavua kuwa amekuwa akimtilia shaka shemeji yake huyo kutokana na kawaida yake kutoka nyumbani pale mumewe anapokwenda kazini.
Shemeji mtu alidadavua kuwa amekuwa akimtilia shaka shemeji yake huyo kutokana na kawaida yake kutoka nyumbani pale mumewe anapokwenda kazini.
“Mkuu kaka akitoka tu kwenda kazini naye
amekuwa na kawaida ya kuchomoka ‘homu’, nahisi kuna harufu ya usaliti.
Nimejaribu kumweleza kaka akaniambia nimfanyie uchunguzi, sasa leo
nilibana sehemu nikamsikia akizungumza kwenye simu masuala ya mapenzi
hivyo namfuatilia,” alisema jamaa huyo.
OFM, baada ya kunyaka taarifa hizo na
kuelekezwa kule anakoelekea mwanamke huyo, walikusanya vifaa vyao na
kuungana na shemeji mtu huyo katika kumfuatilia dada huyo.
Safari ya dada huyo iliishiia katika gesti moja iliyopo Sinza-Mori, Dar, maeneo ya Meeda Club.
Safari ya dada huyo iliishiia katika gesti moja iliyopo Sinza-Mori, Dar, maeneo ya Meeda Club.
Kwa mujibu wa taarifa za mapokezi,
mwanadada huyo alipofika alipitiliza hadi chumbani bila kujua kuwa
shemeji yake pamoja na OFM wanamfuatilia hatua kwa hatua.
Aliyeng’amua chumba alichozama ni dereva wa bodaboda ambaye alitumwa atangulie ndani ya gesti hiyo.
Ndani ya dakika sifuri, dereva bodaboda alirudisha majibu kuwa alimuona akizama chumba namba tano.
Dakika kumi baadaye, OFM ilishauri kuripoti polisi na serikali za mtaa ambapo watu hao walifika na kuongozana kisha kuingia kwenye gesti hiyo.

Baada ya kujitambulisha mapokezi na
kuonesha vielelezo, waliruhusiwa kwenda kugonga chumba namba tano ambapo
jamaa huyo alinaswa laivu akijiandaa kuvunja amri ya sita na mke huyo
wa mtu, kumbe yeye alishatangulia chumbani muda mrefu.
Baada ya jamaa kukutwa utupu na mke wa
mtu, nusura adondoke kwa presha kwani aliangua kilio kama vile
ametangaziwa adhabu ya kifo hasa alipomuona shemeji mtu ambaye kumbe
walikuwa wakifahamiana.
Ndani ya chumba hicho kulitokea sekeseke
la aina yake ambapo sakata hilo lilitinga katika Kituo cha Polisi cha
Kijitonyama, Dar (maarufu Mabatini) kwani shemeji mtu aligoma kulimaliza
kiutu uzima kama mfumaniwaji alivyotaka.
Mpaka OFM wanaondoka kituoni hapo usiku
mnene, waliwaacha wahusika wakiwa katika kikao kizito cha kuwekeana
mambo sawa ili sakata hilo maarufu kama mchepuko liishie hapohapo