Kila kukicha msanii Christopher Mourice a.k.a Chris Brown
amezidi kukumbwa na mikiki ya hapa na pale baada ya kukaa sana
rehab.Tangu ijumaa ya wiki iliyopita alitimuliwa na sasa mahakama
imeamua Chris aende jela mwezi mmoja kuanzia sasa hadi mwezi April 23,
kutokana na kukiuka masharti aliyopewa na mahakama.
Sababu moja wapo iliyompelekea Chris kutimuliwa rehab ni kukataa
kipima kipimo kinachoonesha kama anatumia dawa za kulevya, pia sharti
lingine ambalo amelikiuka alionekana akimshika mwanamke wa rehab hiyo
sehemu ya mkono.
Katika rehab iyo inayoitwa Malibu, sharti moja wapo ni kukaa mbali na
mwanamke yeyote zaidi ya umbali wa hatua mbili, lakini Chris alionekana
kukiuka hivyo ikampasa atimuliwe