Mbunge
wa Chadema John Wenje, aliyewahi kuwaita Wabunge wa CUF kuwa ni
mashoga, leo ameuza kizaa zaa cha ajabu bunge la Katiba baada ya kuwaita
Wajumbe 201 wasiokuwa wabunge kwenye bunge la Katiba Dodoma kuwa ni
wala rushwa na kwamba wamekula rushwa kwa kupewa chakula, soda na bia na
Mawaziri wa CCM. Mwenyekiti wa Bunge alipomtaka atoe ushahidi kama
Sheria inavyosema, alishindwa kuutoa na kuendelea kuleta ubishi wa
kitoto ndipo Mwenyekiti wa Bunge hilo Mh. Mwenyekiti alipomuamuru kwa mujibu
wa Sheria za bunge hilo kuripoti mara moja kwa Kamati ya maadili ya
bunge hilo na huko atatakiwa kuonyesha ushahidi wa tuhuma zake na suala
hilo litarudishwa tena kwenye Bunge hilo kwa uamuzi. |