Katibu mkuu wa chama hicho, Gwede Mantashe, amesema kuwa afisa yeyote
aliyehusishwa na makosa yoyote, lazima akabiliwe na sheria.
Lakini amepuuzia mbali wito wa
Rais Zuma kuondolewa mamlakani kwa kura ya wabunge au hata kujizulu.
Hapo jana mdhibiti wa mali ya umma,Thuli Madonsela, alisema kuwa Zuma
alitumia sehemu za pesa za umma zilizotengewa ukarabati wa nyumba yake
kwa mambo yake binafsi.
Thuli Madonsela, aliamuru Rais Zuma kulipa pesa za ziada alizotumia
za umma kukarabati nyumba yake ya kifahari, akisema kuwa alijinufaisha
na pesa za umma kwa njia isiyofaa.
Ukarabati huo, ulijumuisha bwawa la kuogelea, kliniki binafsi na eneo la helikopta kuweza kutua.
Chama hicho kimesema kuwa ripoti hiyo imetolewa wakati usiofaa nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi Mei.
SOURCE: BBC