Jose
Mourinho amekataa mwaliko wa kutafuta suluhu na mpinzani wake wa siku
nyingi kocha Roberto Mancini kwa kukataa hadharani mualiko wa chakula
cha usiku baada ya mechi ya Chelsea vs Galatasary.
Chelsea wanaikaribisha Galatasary inayofundishwa na Mancini leo
kwenye uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo wa pili wa raundi ya 16
bora.
Makocha hao wawili wamekuwa wakilumbana mara kwa mara tangu Mourinho
alipomrithi Mancini kama ukocha kwenye klabu ya Inter Milan mwaka 2008
hasa baada ya Mancini kujitamba kwamba alichangia kwa kiasi kikubwa
katika kuisuka timu ya Milan iliyokuwa ikifundishwa na Mourinho na
kuweza kutwaa makombe manne mwaka 2010.
Katika
mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi, Mancini alisema
angelipia chakula cha usiku na Mourinho ikiwa Galatasary itashinda mechi
ya leo lakini wakati Mourinho alipoulizwa kama amekubali mualiko wa
Mancini, alitingisha kichwa chake na kusema “hapana”.
‘Kwa sababu sihitaji kufanya jambo baada ya mechi, sifanyi vitu kwa
sababu nimeshinda au nimefungwa baada ya mechi kilichopo kichwani ndio
nakifanya haijalishi nimeshinda au nimefungwa, sitoweza kwenda kula
chakula cha usiku na mtu fulani ambaye ana kazi yangu, na kitu pekee
kinachotufananisha ni kwamba wote ni makocha wa timu za soka