Ni
moja ya taarifa ambazo nimezisikia sana kwa wiki hii hapa Nairobi
inayosema kuhusu Mchungaji mmoja maarufu kwenye mji huu kwa
jina la Geofrey Maingi wa kanisa la Redeemed Gospel alikutwa amefariki kwenye chumba cha kulala cha mama ambae ni muumini wake huko Buruburu.
jina la Geofrey Maingi wa kanisa la Redeemed Gospel alikutwa amefariki kwenye chumba cha kulala cha mama ambae ni muumini wake huko Buruburu.
Vyombo mbalimbali vya Kenya vimeripoti kwamba kwamba marehemu aliekua
na umri wa miaka 70, alikua amekwenda nyumbani kwa mama ambae ni
muumini wake kwa lengo la kumfanyia maombi lakini akafariki wakati
maombi yakiendelea.
Mama huyu ambae amesema ana umri wa miaka 40, amewaambia Polisi
kwamba Marehemu alizirai wakati wakiwa kwenye maombi na kwamba
hawakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi japo majirani wanasema wawili
hawa walikua wapenzi.
Baadhi ya mashuhuda wanasema Mchungaji huyu amekua na kawaida ya
kwenda kwenye nyumba ya huyu mama kila weekend, na mara nyingi amekua
akienda Jumamosi na kuondoka Jumatatu.
Mke wa Marehemu alizimia baada ya kupata taarifa za kifo cha mume
wake ambacho kimetokea wiki mbili baada ya mchungaji mwingine wa Embu
kufumaniwa na mke wa mtu.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako