A

A

Theruji Iliyoanguka hii leo Nchini Marekani ni Noma,Picha hizi hapa.

 Mpita njia akipita kwenye lundo la theluji iliyowekwa pembeni baada ya magari ya plao kuisogeza kwa ajili ya kusafisha njia ya magari ili yaweze kupita bila matatizo yeyote, theluji iliyoanguka DMV ni kuanzia inchi 8, mpaka 18 na majimbo mengine yaliyoathirika na theluji hii ni pamoja na North Carolina, Alabama, Georgia, kwa wanaosafiri leo wanatakiwa wawe waangalifu na kama huna safari ya uzalima umeshauliwa utulie nyumbani kama kama utalazimika kutoka hakikisha unamafuta ya kutosha kwenye gari na wanaosafiri na anga unatakiwa upige simu kwanza kwa sababu usafiri wa anga sehemu nyingi umesitishwa.
 Maeneo ya Beltsville, Maryland katika picha.
 Maeneo ya I 95 N yalivyokua yakionekana leo baada ya theluji kuanguka usiku wa kuamkia leo Alhamisi maeneo ya DMV
 Pamoja na kwamba hakuna kazi sehemu nyingi zikiwemo ofisi za serikali na shule magari ya kubebea wagonjwa yapo kazini kama kawaida zikiwemo sehemu muhimu kama mahospitalini na kwengineko.
 Maeneo Denton, Maryaland.
 Barabara nyingi kubwa wamejitahidi sana kusafisha.
 Juu na chini ni maeneo ya Denton wakaazi wakijaribu kuondoa theluji iliyozuia magari yao yalio kwenye maegesho ya nyumba wanazoishi
Credit to Vijimambo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako