A

A

Taarifa za Awali Kuhusu Kunusurika Kulipuliwa kwa Ofisi za Chadema Makao Makuu

Quote By Tumaini Makene View Post

Kumekuwa na jaribio la kulipua Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni majira ya saa 8 usiku wa leo Februari 11.

Maelezo ya awali yanaonesha kwamba watu waliofanya tukio hilo walifika maeneo ya ofisi wakiwa na gari ndogo ambayo plate number zake zilikuwa zimezibwa.

Wakapaki kama vile wanaendelea na shughuli kwenye 'ofisi' nyingine iliyo jirani na Makao Makuu, kisha mmoja wao akatoka nje ya gari na kuelekea kwenye hiyo ofisi ya jirani.

Gari lile liliendelea kuwa pale kwa muda hadi walinzi walipoanza kulishuku na kulifuatilia, ghafla mmoja aliyekuwa ndani ya gari akasikika akisema 'tayari...twende zetu...', aliyekuwa ameshuka kwenye gari kumbe alikuwa ana-guard wenzake waliokuwa wakiwasha moto.

Wakati walinzi wanaanza kuwafuata kuchukua hatua za kuwadhibiti, gari lile likaondolewa kwa kasi huku likimkosa kosa kumgonga mtu mmoja.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama (DSI), Wilfred Muganyizi Lwakatare anasema kwa namna tukio hilo lilivyoendeshwa, lilikuwa na malengo ya kulipua Ofisi za CHADEMA Makao Makuu.

Anasema siasa za Tanzania sasa zinaelekea sehemu mbaya kama Serikali, kupitia vyombo vya dola, vitaendelea kuchukulia mzaha au kutochukua hatua madhubuti dhidi ya matukio ya namna hii, akikumbushia matukio mengi, mengine yakihusisha silaha za kivita, yakiilenga CHADEMA au viongozi wake, kwa nia ya kukisambaratisha, baada ya watawala kushindwa kutumia ushawishi wa kisiasa kwa sera na hoja mbalimbali.

Tukio hilo limetolewa taarifa polisi.
Chanzo:Afisahabari wa Chadema TUMAINI MAKENE/Jamiiform

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako