Wanasoka
wenye jinsia ya kike nchini Iran hivi sasa wanatakiwa kabla ya
kushiriki kwenye mechi za mchezo huo kufanyiwa vipimo vya kugundua
jinsia – hatua hii imekuja baada ya wanasoka kadhaa nchini humo –
wakiwemo wanne kutoka katika timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Iran
kugundulika kuwa walikuwa ni wanaume.
Wachunguzi wa kitabibu watakuwa
wanavamia bila taarifa katika mazoezi
ya timu za wanawake zinazoshiriki katika ligi kuu ya soka la wanawake
nchini humo ili kujaribu kuwagundua wanawake wanaojifanya wanawake na
kucheza pamoja.
Pia imewekwa sheria mpya ya kuvilazimisha vilabu kufanya vipimo vya
afya ya jinsia kwa wachezaji wapya kabla ya kuwasajili kimikataba, hii
ni kwa mujibu wa Ahmad Hashemian, mkuu wa shirikisho la soka la Irani
kwenye upande wa kamati ya afya.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako