SIMU ya Kichina imezua balaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Jumatano iliyopita wakati wa usikilizwaji wa kesi ya Katibu wa Jumuiya ya Kiislamu, Shehe Ponda Issa Ponda, Ijumaa linakupa habari kamili.
Tukio hilo la aina yake lilitokea baada ya simu ya Kichina ya mmoja
wa wafuasi wa Shehe Ponda aliyefahamika kwa jina la Shehe Kitula kuita
wakati shughuli za kimahakama zilizopokuwa zikiendelea.
Wakati jaji wa mahakama hiyo, Augustino Mwalija akitahamaki kwa
kitendo hicho, askari waliokuwepo mahakamani hapo walimkamata Shehe
Kitula anayeswali katika Msikiti wa Masjidi Haki uliopo Buguruni jijini
Dar na kwenda kumhoji.
Baadhi ya waumini walipinga kitendo cha Shehe Kitula kukamatwa na
kutaka kufanya fujo ili asiingizwe kwenye chumba cha mahojiano lakini
walitulizwa na wenzao.
Shehe Kitula alipohojiwa na waandishi wetu alikiri kuchanganywa na
simu hiyo baada ya kusahau kuizima alipoingia mahakamani hapo.
“Nilisahau kuizima simu, polisi walikuwa na haki ya kunikamata kwa kuwa sheria hairuhusu kelele mahakamani,” alisema shehe huyo.
Kesi ya msingi, Shehe Ponda anashtakiwa na serikali kwa kosa la kutoa
lugha za uchochezi alipokuwa akihutubia moja ya mikutano yake ya
hadhara mjini Morogoro mwaka jana.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 26, mwaka huu ambapo mwanasheria
wa serikali atatakiwa kujibu hoja za mwanasheria wa Shehe Ponda, Juma
Nassoro.
Wakati huo huo, Jaji Mwalija anaweza kumpa dhamana Shehe Ponda au kumnyima.
>>GPL
>>GPL
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako