Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa Khamis M. Mgeja alienda kumpa pole Afisa Mtendaji wa kata
ya Ubagwe katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu Alphonce John Kimario aliyejeruhiwa kwa kushambuliwa na mapanga na watu aliowataja kuwa ni wafuasi wa Chadema.
Hii
inasemekana kutokana na vurugu zilizotokea jioni ya February 04,majira
yakiwa ni saa 1 usiku katika kata ya Ubagwe muda mfupi baada ya
kumalizika kwa kampeni za kumnadi mgombea wao.
Akizungumza
na waandishi wa habari Afisa huyo Mtendaji wa kata ya Ubagwe Alphonce
John Kimario amesimulia kuwa pamoja na kuumia vibaya machoni hasa jicho
lake la kulia pia analalamika juu ya maumivu makali.
Maumivu anayodai kuyasikia kwa sasa Kimario yapo sehemu za mgongoni
na hii ni mara baada ya kupigwa na nondo ambapo kwa hivi sasa upande wa
kulia pamoja na bega lake umekufa ganzi Kimario ambaye amepigwa
nondo,mapanga na kwenye paji la uso kiasi cha kushonwa nyuzi kadhaa na
kutobolewa jicho moja kwa sasa amekimbizwa hospitali ya Rufaa Bugando
kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi.
Majeruhi wengine kama Masoud Melimeli (katibu Mwenezi wa Wilaya)
amebaki katika uangalizi wa Hospitali ya Wilaya akiwa na majeruhi
wengine kama Ramadhani Salum (Umoja wa Vijana) na Mussa Daudi (Katibu
Uchumi Kata ya Nyihogo) ambaye alilazwa katika Hospitali ya wilaya ya
Kahama na mara baada ya kuzidiwa amepakiwa kwenye Ambulance na
kuwahishwa Bugando kwa ajili ya matibabu zaidi.
chanzo:Bofya hapa
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako