NAPE NNAUYE |
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na
kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani
uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23.
Akitoa shukrani hizo, Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo kwamba siri ya CCM
kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba,
kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania
wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.
Nape alisema CCM inaahidi
kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina
uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa
wananchi.
Akizungumzia kushindwa kwa
CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye
kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta
tatu na kuambulia kata tatu.
"CHADEMA wamevuna walichopanda
Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa
wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania
hawakiamini," alisema.
Katika uchaguzi huo CCM
ilishinda katika kata CCM ilishinda katika kata 23 za Kibindu na
Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga),
Ibumu na Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara),
Malindo, Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na
Ludewa (Morogoro) na Mrijo (Dodoma).
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako