Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika
ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.Nape alisema kitendo cha wana CCM
kushambuliwa ni kitendo cha kinyama na kinatakiwa kikemewe na kila
mtu,pia alisisitiza Vijana wa CCM kuwalinda wapigaji kura wao siku ya
kupiga kura.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake
na waandishi wa Habari kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitazama picha ya X-Ray ya Sebastian
Masonga Katibu wa UVCCM kata ya Majengo Wilaya ya Kahama,Masonga
amevunjika mkono wa kushoto baada ya kupigwa na wafuasi wa Chadema
wakati walipokua wanarejea kwenye mikutano ya kampeni za Udiwani.
Katibu wa NEC
Itikadi na uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akimpa pole Afisa Mtendaji wa
Kata ya Ubagwe wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambaye alipigwa na
kutobolewa macho na wafuasi wa Chadema .
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoka nje ya jengo la hospitali ya
Bugando akiongozana na baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza ambapo
waliwatembelea na kuwajulia hali majeruhi walioumizwa na wafuasi wa
Chadema mjini Kahama





No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako