CCM wavuruga kijijini kwa Mbunge Selasini
Kwa ufupi
- Akiwapokea wanachama hao wapya, Katibu Mwenezi wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, Michael Mwita, alisema hatua ya wananchi hao kurudi kwenye chama hicho inaonyesha jinsi walivyochoshwa na siasa za mbunge wao.
Rombo. Chama Cha Mapinduzi
(CCM) katika Wilaya ya
Rombo, kimeitikisa ngome ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (NCCR-Mageuzi), baada ya zaidi ya wananchi 140 katika
Kijiji cha Makiidi, ambako ndiko nyumbani kwa mbunge huyo kujiunga na chama hicho.
Akiwapokea wanachama hao wapya, Katibu Mwenezi wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, Michael Mwita, alisema hatua ya wananchi hao kurudi kwenye chama hicho inaonyesha jinsi walivyochoshwa na siasa za mbunge wao.
Wananchi 52 kati yao walikabidhiwa kadi za CCM na wengine 60 walikabidhiwa kadi za Umoja wa Vijana (UVCCM) wakati 25 walikabidhiwa kadi ya Umoja wa Wazazi wa CCM na 10 walikabidhiwa kadi ya chipukizi. Mwita alisema tatizo la CCM kwa sasa ni baadhi ya watu kutofuata katiba ya chama na kwamba kama hilo litaondoka, hakuna chama chochote kitakachoweza kuigusa CCM.
Alisema ni vyema kila mwanachama na kiongozi kujua majukumu yake na kuyatimiza badala ya kunung’unika kupitia katika mikusanyiko iliyoko nje ya utaratibu. Katibu mwenezi huyo alisema CCM kwa sasa haitamfumbia macho mtu yeyote wakiwemo viongozi wasiofuata taratibu.
Wakizungumza baada ya kuapa kujiunga na CCM baadhi ya wananchi hao walisema wamechoshwa na sera zisizotekelezeka.

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako