Mabingwa
wa Tanzania bara klabu ya Dar Young Africans leo imetoa kipigo cha mbwa
mwizi kwa klabu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
uliochezwa uwanja wa taifa Dar es salaam.
Katika mchezo huo ulioisha hivi punde mabao ya Yanga yalifungwa na
mshambuliaji Didier Kavumbagu katika sekunde ya 40 ya mchezo, kabla ya
Msuva kufunga bao la pili katika dakika ya pili.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda aliyeanza kuichezea Yanga leo
tangu apewe ruhusa na Fifa, Emmanuel Okwi akaziona nyavu za Ruvu katika
dakika ya 27, dakika 3 baadae Mrisho Ngassa akaipatia Yanga bao la 4.
Hadi timu zinaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Kipindi cha pili Yanga wakarudi kwa kasi na kufanikiwa kuongezea
mabao mawili yaliyofungwa na Kavumbagu tena, Hamisi Kiiza na Saimon
Msuva akafunga hesabu kuhitimisha ushindi wa mabao 7-0.
Wakati huo huo timu ya Mbeya City nayo imefungwa 2-0 na Coastal Union
katika mchezo uliochezwa huko Mkwakwani Tanga. Mabao ya Coastal
yamefungwa na Mohamed Mtind
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako