MATAPELI HAO WALIUTUMIA MGAHAWA WA FRESH COACH KUTAPELI..!

Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya leo, Februari 20.

Bi. Shembusho akilia kwa uchungu baada ya kudanganywa na watu wawili, wa kike na wakiume ambao majina yao bado hayajafahamika. watu hao walimpeleka katika Hoteli maarufu mjini moshi, Fresh Coach na kumtapeli shilingi milioni 5.4 ambazo alikuwa ametoka kutoa Benki ya Uchumi ya mjini Moshi.

Askari wa Hoteli hiyo inayodaiwa kutumika kumtapeli mwanamke huyo akimtuliza Mama huyo ambaye alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo.
Msamaria Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.
Mama akisimulia tukio zima kwa wananchi waliofika katika eneo la tukio baada ya kumsikia akipinga ukunga kuomba msaada.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako