Mh. Khalfani Barwany Mb jimbo la Lindi akiongea na waandishi wa Habari. (Hawapo pichani, Picha na Maktaba)
*******
Baada
ya Kupata taarifa za Chama cha Wananchi C.U.F kumvua uanachama ndg
Abdallah Khatau aliyekuwa diwani wa Kata ya makonde Manispaa ya Lindi
kwa Kosa la UTOVU WA NIDHAMU ANAOUONYESHA NDANI YA CHAMA HICHO uliamua
kutafuta ukweli wa hilo lililokuwa likisemwa na baadhi ya wananchi wa
Manispaa hii. Minongono hiyo ilianza hapo jana katika mkutano wa Mh.
Mbunge alioufanya katika Manispaa hiyo ya Lindi.
Mtandao wetu uliweza kuongea na Mh. Mbunge wa Jimbo la Lindi na kusema
ni kweli ndg Abdallah Khatau amevuliwa uanachama wa chama cha Wananchi
C.U.F kupitia kikoa cha kamati tendaji cha Manispaa ya Lindi ya Chama
Hicho na Kufikia uamuzi wa Kumvua uanachama Diwani huyo wa Kata ya
makonde, Hata hivyo aliongeza kuwa Chama Hicho kimetoa Onyokali kwa
Diwani wa Mitandi Ndg Hafidhi Chitutu Baada ya Kuomba radhi chama hicho
kwa kile kile kinachosemwa ni Utovu wa Nidhamu. Hayo yamethibitishwa na
Mbunge wa jimbo la Lindi Mh. Salum Khalfan Barwany, alipoongea na
Lindiyetu.com Chama hicho kinajiandaa kuwasilisha taarifa rasmi kwa
Mkurungezi wa Manispaa ya Lindi ya Kuwa nafasi ikowazi katika kata hiyo
hivyo yawezekana uchaguzi mdogo kufanyika hivi karibuni.
credit: Lindiyetu.com
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako