Msanii
wa filamu Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama Lulu (pichani)
anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake
Steven Kanumba (28), anatarajia kujibu mashitaka yake kwa mara ya
kwanza Februari 17, mwaka huu katika Mahakakama Kuu Tanzania, Kanda ya
Dar es Salaam. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji na bila
kukusudia, iliyotolewa na Mahakama Kuu kwa kanda hiyo, kesi ya Lulu
itasikiliza mbele ya Jaji Rose Teemba na mshtakiwa atajibu mashitaka
yake kama ni kweli au siyo kweli.Aidha ratiba hiyo inaonyesha kwamba
mshtakiwa akisomewa mashtaka na kujibu, mahakama itapanga tarehe ya
kusikiliza maelezo ya awali dhidi ya kesi hiyo.
Mnamo
Januari 29, mwaka 2013 Lulu aliachiwa kwa dhamana baada ya kesi hiyo
kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda
mauaji ya bila kukusudia.
Aidha,
Lulu alipata dhamana hiyo baada ya Jaji Zainabu Mruke kutoa masharti
ya dhamana kwa mshtakiwa huyo baada ya wakili wa utetezi Peter Kibatala
kuwasilisha maombi ya dhamana kwa hati ya dharula chini ya kifungu cha
148 kidogo cha (1) na cha (2) cha Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai
(CPA). Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Joseph Maugo
na Kishenyi Mutalemwa.
Wakili
Kibatala alidai kuwa hati hiyo imeambatanishwa na hati ya mashtaka
yanayomkabili Lulu la kuua bila kukusudia na kwamba kwa mujibu wa shtaka
hilo mshtakiwa ana haki ya kupata dhamana.
Upande
wa Jamhuri, ulidai kuwa hauna pingamizi la maombi hayo na kwamba
mahakama ijielekeze kwenye kifungu cha 148 kidogo cha (6)ambacho
kinamtaka mshtakiwa kufuata masharti yatakayotolewa chini ya kifungu
hicho.
Jaji
Mruke alisema kosa linalomkabili mshakiwa lina dhamana kisheria na
kwamba mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kufuata masharti ya kuwa na
wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali watakaosaini hati ya
dhamana ya Sh. milioni 20 kila mmoja.
"Tukubaliane
wote kwamba hakuna ubishi roho ya mtu imepotea hivyo sheria lazima
ifuatwe... pia mshtakiwa awasilishe hati zake za kusafiria, kuripoti
kila tarehe Mosi ya mwezi kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha msajili
huyo" alisema Jaji Mruke.
Alisema Msajili wa Kanda ya Dar es Salaam ahakiki masharti ya dhamana kabla ya mshtakiwa hajaachiwa kwa dhamana.
Katika
kesi ya msingi, Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka Sinza Vatican,
jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Kanumba bila kukusudia.
MICHUZI MEDIA GROUP

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako