Mario Balotelli alionekana akitokwa na machozi usiku wa mchezo wa
ligi kuu ya Italia kati ya timu yak AC Milan dhidi ya Napoli, hali hii
ilitokea baada ya kutolewa uwanjani zikiwa zimebakia dakika 15 kabla ya
mchezo kuisha.
Baada ya Adel Taarabt kuifungia Milan bao la kuongoza katika dakika
ya 8 tu ya mchezo, Gökhan Inler akaisawazishia Napoli kabla ya Gonzalo
Higuain kufunga mabao mengine ya ushindi yaliyomtoa machozi Super
Mario.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako