A

A

Huu ndio Ujumbe aliotumwa Mh:Sumaye akampelekee Mh:Lowassa kuhusu 2015

Wanafunzi wa vyuo jijini Mwanza waonyesha mahaba yao kwa MH Lowasa wamtua MH. Sumaye afikishe salamu zao


Waziri mkuu mstaafu Mh.fredrik Sumaye amesema kuna haja ya kuwa na uwiano wa umiliki wa kibiashara kati ya kampuni za nje na za Ndani ili kukuza uchumi wa nchi.
Sumaye ameyasema hayo leo wakati wa kongamano la ajira na maendeleo kwa Vijana lililoandaliwa na chuo cha biashara  tawi la Mwanza likiwashirikisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali kutoka Mwanza.
Amesema katika  uwiano huo lazima kuwepo umiliki wa kutosha kwa kampuni za Ndani kwa ajili ya ukuaji wa haraka wa kiuchumi kwa taifa na  jamii kwa ujumla.
Aidha amefafanua kuwa kunapaswa kuwapo kwa mgawanyo sahihi kwa kampuni na si dhana ya kampuni za nje kutowekeza ndani ya nchini bali ni kwa mustakabali wa uwiano wa kujenga uchumi imara.

Katika kongamano hilo pia Sumaye amewasisitiza vijana kujifunza ujasiriamali ili kuepukana na changamoto za ajira hususani suala la kilimo ili kukabiliana na uhaba wa upatikanaji wa chakula nchini.
                IMEANDIKWA NA Shadrack Mgaya  
 Hapa ni baadhi ya washiriki kwenye kongamano lilofanyika katika ukumbi wa nyanza jijini mwanza washiriki walikuwa wanafunzi wa vyuo jijini mwanza
 Mh. Sumaye akizungumza katika kongamano hilo leo








 waandishi wa habari nao hawakuwa nyuma katika kongamano hiliwalikuwepo na walifuatilia kwa makini pia


 Baadhi ya wageni waalikwa waliokuwepo katika kongamano hilo wakiwa wanafuatilia kwa makini kabisa
 Baadhi ya wageni waalikwa waliokuwepo katika kongamano hilo wakiwa wanafuatilia kwa makini kabisa



 Baadhi ya wageni waalikwa waliokuwepo katika kongamano hilo wakiwa wanafuatilia kwa makini kabisa

 Viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakiwa wanafuatilia suala hili kwa makini kabisa


 Hapa vijana waliamua kuonyesha waziwazi mahaba yao kwa mh.Lowasa na kutuma salamu kwake kama unavyoona bango hili


No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako