A

A

Hii ndio bajeti ya Manispaa ya Kinondoni Zaidi ya Bilioni 121 zatengwa Miradi ya Maendeleo 2014


 
Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni limepitisha bajeti ya sh.bilioni 121 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015. 
Akitoa taarifa hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Yusuph Mwenda alisema fedha hizo zimetokana na makusanyo ya vyanzo vya mapato , pesa kutoka ruzuku serikali kuu,Tamisemi,pesa za makusanyo ya ndani ya Halmashauri .
Kwa sasa Halmashauri ina uwezo wa kujiendesha kwa asilimia 30 tofauti na hapo nyuma ambapo ilikuwa ikijiendesha kwa asilimia 20 tu. 
Bajeti ya mwaka 2014/2015 ina lengo la kutekeleza mipango ya maendeleo na kuwaondolea umaskini wakazi wa kinondoni na kuboresha maisha yao.Imetolewa na Manispaa ya Kinondoni. 
CHANZO: MTAA KWA MTAA

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako