Daktari feki akamatwa akiwa na baadhi ya kadi za wagonjwa na vipimo.
Hospitali
ya taifa Muhimbili imemkamata
daktari feki hospitalini hapo asubuhi ya tarehe ishirini na tano akiwa na baadhi ya kadi za wagonjwa na vipimo huku historia yake ikionesha aliwahi kuajiriwa na serikali kama utabibu katika hispitali ya amana na Mwananyamala kabla ya kuacha kazi mwaka 1997.
daktari feki hospitalini hapo asubuhi ya tarehe ishirini na tano akiwa na baadhi ya kadi za wagonjwa na vipimo huku historia yake ikionesha aliwahi kuajiriwa na serikali kama utabibu katika hispitali ya amana na Mwananyamala kabla ya kuacha kazi mwaka 1997.
Akitoa taarifa za kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo
afisa uhusiano mwandamizi wa hospitali hiyo Bw. Aminieli Aligaesha
amemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la Kitano Kitani mwenye umri wa miaka
52 ambaye alijifanya daktari upande wa wazazi alikamatwa bada ya
kujaribu kuwatapeli watu mbalimbali hospitalini hapo na amekuwa
akionekana mara kwa mara na wagonjwa wengi walidhani kuwa yeye ni
daktari halali.
Mtuhumiwa huyo licha ya kukiri kufanya kazi ya
utabibu kwa miaka mingi amekana kuhusika na tukio lolote la utapeli
hospitalini hapo na kubaini amekuwa akifika hospitalini hapo kwa mambo
yake binafsi na kukiri kuendelea kutoa huduma mtaani mara baada ya
kuacha kazi ya utabibu.
Raisi wa chama cha madaktari Tanzania daktari
Primas Saidia amekiri ongezeko la madaktari feki kwenye hospitali
mbalimbali nchini na kushindwa kuthibitisha moja kwa moja kama
wanashirikiana na madaktari halali kwenye hospitali husika na kuwa
tayri wamejipanga kupambana na matukio hayo kwa kuwapa madaktari mihuri
na makoti maalimu yenye nembo ili kuwafanya wagonjwa kutambua nani
daktari halali ama la.
ITV
ITV
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako