Mbio za kuwania ubunge katika Jimbo la Kalenga unabaki kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kuthibitisha kutosimamisha mgombea.
Naibu
Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa CUF, Abdul Kambaya, amesema
chama chake hakina mpango wa kusimamisha mgombea katika jimbo hilo na
kwamba hivi sasa wanaandaa mikutano ya kuimarisha chama chao.
“Mpaka
sasa CUF haina mpango wa
kusimamisha mgombea ubunge Kalenga… kwa sasa tunaandaa kikao cha Kamati Tendaji kitakachokaa kati ya Februari 15 na 16 mwaka huu ili kujadili masuala mbalimbali,” alisema Kambaya.
kusimamisha mgombea ubunge Kalenga… kwa sasa tunaandaa kikao cha Kamati Tendaji kitakachokaa kati ya Februari 15 na 16 mwaka huu ili kujadili masuala mbalimbali,” alisema Kambaya.
CHADEMA
imepanga kumtangaza mgombea wa kiti hicho wakati wowote baada ya Kamati
Kuu ya chama hicho kuketi mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya kuteua
jina la mgombea.
“Kwa
sasa chama kinakusanya fomu za waliojitokeza kugombea jimbo hilo… hadi
sasa tunaendelea na zoezi hilo, mwamuzi wa mwisho ni kamati kuu
itakayoketi mwisho wa mwezi huu kwa ajili ya uteuzi wa jina hilo,”
alisema Ofisa Habari wa Chama hicho, Tumaini Makene.
Juzi
CCM ilimtangaza Godfrey Mgimwa, mtoto wa aliyekuwa mbunge wa Kalenga na
Waziri wa Fedha na Uchumi, marehemu William Mgimwa, kugombea katika
uchaguzi mdogo, ambao kampeni zake zitaanza rasmi Februari 19, mwaka
huu.
Mgimwa
alichaguliwa kwa kura 348 za maoni za wajumbe 708 kati ya wajumbe
halali 816 wa CCM katika mkutano mkuu wa jimbo hilo, na aliibuka kidedea
kati ya wagombea tisa waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
chanzo:HAPA
chanzo:HAPA
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako