Ubalozi wa Marekani Kampala wasema kuna ishara kwamba jumba la makumbusho la kitaifa ni mojawapo ya majengo yanayolengwa na magaidi
Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umeonya juu ya uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi katika mji mkuu wa Kampala.
Katika ujumbe uliotolewa Jumatatu jioni, ubalozi huo ulisema umepata habari kwamba huenda kundi la washambuliaji likiwa tayari kuvamia malengo kadhaa mjini Kampala mwezi Februari na Machi.
Taarifa hiyo inaongeza kuwa kuna
ishara kwamba jumba la makumbusho la kitaifa ni mojawapo ya majengo
yanayolengwa. Lakini serikali ya Uganda haijatoa tamko la haraka juu ya
onyo hilo.
Ujumbe huo haujawaonya Wamarekani
kuondoka Kampala lakini umewatahadharisha kuepuka jumba la makumbusho na
maeneo mengine yenye watu wengi.
Kundi la al-Shabab kutoka Somalia lilifanya shambulizi la kigaidi huko Kampala Julai 2010 na kuuwa watu 70.
Chanzo, voaswahili.com
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako