Usiku wa kuamkia Jumatatu wezi
wanaodhaniwa kuwa mashabiki wa klabu ya Borrusia Dortmund wamemfanyia
kitu mbaya mshambuliaji klabu hiyo Robert Lewandoski baada ya kuifanya
gari la mshambuliaji huyo kuwa ‘screpa’ kwa kuiba matairi yote ya gari
hiyo.
Gari hilo aina ya Porsche Cayenne lilikuwa limepaki nje ya nyumba ya mshambuliaji huyo huko Ujerumani, wezi waliiba matairi yote na kuliacha gari hilo juu ya mawe. Kwa mujibu wa gazeti la Bild, sasa itamgharimu Lewandowski kiasi cha €2,500 kuweza kuifanya gari hiyo itembee tena
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako