Mkuu
wa Wilaya ya Kilolo,Mh.Gerald Guninita akifungua kikao cha DCC katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya,Kushoto ni Mkurugenzi Ruukia Muwango na
Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya,kikao kilichofanyika
mwisho mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi
wa wilaya ya Kilolo Rukia Muwango akisoma taarifa ya wilaya hiyo mbele
ya wajumbe wa kamati ya wilaya katika kikao kilichofanyika katika ukumbi
wa wilaya mwishoni mwa wiki.
======== ======= =======
Na Denis Mlowe,Kilolo
JUMLA
ya wanafunzi 1725 waliotakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza
katika shule mbalimbali zilizoko katika Wilaya ya Kilolo wameshindwa
kuripoti kutokana na sababu mbalimbali.
Akizungumza
katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika
katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo mwishoni mwa wiki,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Rukia Muwango alisema
wanafunzi wasioripoti kati ya hao wavulana walikuwa 788 na wasichana 937
sawa na asilimia 56.1
Muwango
alisema wanafunzi waliochaguliwa kwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ni
wanafunzi 3101 wavulana 1442, wasichana 1658 kati ya hao wavulana 10 na
wasichana 10 wamechaguliwa katika shule za bweni.
Alisema
wanafunzi waliopangwa kwenda katika shule za ufundi walikuwa wavulana 6
na hakuna msichana aliyechaguliwa na wanafunzi 3074 walipangwa katika
shule za serikali katika halmashauri ya wilaya ya Kilolo.
Aliongeza
kuwa wanafunzi walioripoti hadi Januari 23 mwaka huu walikuwa wanafunzi
1349 wakiwemo wavulana 638 na wasichana 711 sawa na asilimia 43.
Muwango
alizitaja shule ambazo zina asilimia ndogo ya wanafunzi walioripoti
shuleni kuwa ni shule ya Sekondari Mawambala (5.2%), Mlafu (14%), Lukosi
(19.3%),Udekwa (21%) na Mtitu yenye asilimia 29 ya wanafunzi
walioripoti.
Aliwataka
walimu wa wakuu shule za sekondari wawasilishe majina ya wanafunzi wa
kidato cha kwanza 2014 waliojiunga katika shule zao ili halmashauri
iweze kujua na kujiridhisha kuwa wanafunzi wote wapo shuleni na kutoa
taarifa kwa wanafunzi wanaokwenda shule za zisizo za serikali kupata
takwimu sahihi.
Alisema
kuwa halmashauri imeandaa mikakati kwa wanafunzi wasioripoti kwa
kuwaandikia barua waratibu wote kuwafatilia wanafunzi hao na kuwahimiza
kuhudhuria katika shule walizopangiwa.
Kwa
upande wa ke Mkuu wa Wilaya hiyo Gerald Guninita amewataka watendaji
wawasisitize wazazi kuwapeleka watoto shule bila kujali suala la ada na
sare za shule.
Aliwataka
watendaji kupeleka ripoti ndani ya siku 24 kwa wanafunzi wote ambao
hawajaripoti shuleni hadi sasa katika ofisi ya wilaya na kuwachukulia
hatua wazazi wakaidi.
“Haki
ya mtoto kupata elimu ni muhimu sana na tusiache wazazi wanaowaficha
watoto ndani hivyo wabanwe wazazi wao kwa kuwaficha kuna kitu nataka
kuwaambia kumpeleka shule mtoto ni kumwongezea thamani mtoto na mzazi
mwenye katika maisha yetu ya kila siku hivyo nawsisitiza sana watendaji
wabaneni sana wazazi wote wasiotaka kuwapeleka watoto wa kike shule”
alisema Guninita

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako