A

A

Visa na Mikasa,Kaburi la Fukuriwa na Maiti ikanyofolewa Uti wa Mgongo huko BUnda

WATU wasiofahamika wamefukua kaburi la Rosa Kikwe, aliyefariki dunia mwaka 2005 na kuchukua mfupa wake wa uti wa mgongo, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina. Jeshi la Polisi Wilaya ya Bunda, limethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi, katika Kijiji cha Kihumbu, Kata ya Hunyari.

Ilielezwa usiku wa tukio hilo, watu hao walifukua kaburi alimozikwa mwanamke huyo, bila ya ndugu wa marehemu kuwa na taarifa yoyote.

Ofisa mmoja wa polisi, ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa sababu si msemaji, alisema baada ya watu hao kuchukua kiungo hicho, walilifukia tena kaburi hilo na kisha wakatokomea kusikojulikana.

“Watu wasiofahamika walifukua kaburi la mwanamke huyo aliyefariki dunia mwaka 2005 na kuchukua mfupa wa uti wa mgongo kwa imani zinazodaiwa ni za kishirikina,” alisema ofisa huyo.

Ilielezwa kesho yake ndugu wa marehemu walipokuta hali hiyo waliingiwa na hofu na kuhisi mwili wa ndugu yao umechukuliwa na ndipo wakatoa taarifa polisi.

Polisi walisema baada ya kuchukua kibali mahakamani, waliongozana na daktari na kufukua kaburi hilo na baada ya kufanya uchunguzi waligundua kuwa mfupa wa uti wa mgongo umechukuliwa.

>>mtanzania

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako