Akidhibitisha
taarifa hiyo, kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema
mwanamke huyo alikamatwa Januari 8, kufuatia ushirikiano ulioonyeshwa
na majirani zake baada ya kupata taarifa ya tabia yake hiyo ambayo
inaelezwa amekuwa akiifanya kwa muda mrefu.
Mwanamke
mmoja aliyefahamika kwa jina la Aretas Joseph, (48), mkazi wa kijiji
cha Lesoroma tarafa ya Useri, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro,
amehojiwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufanya mapenzi na watoto
wadogo wa kiume, wenye umri kati ya miaka 9 na miaka 14, jambo
linaloelezwa kuwa ni shambulizi la aibu.
“Kufuatia
taarifa walizokuwa nazo majirani hao, waliweka mtego
hadi walipofanikiwa kumkuta chumbani kwake akiwa na watoto watatu wa
kiume akifanya nao mapenzi,” alisema.
Alisema
mara baada ya majirani hao kumvizia na kumfuma mama huyo, walitoa
taarifa polisi na mama huyo kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha
polisi cha Rombo.
Kulingana
na taarifa ya kamanda huyo wa Polisi, watoto hao baada ya kuojiwa
walisema kuwa wapo Wanne na siku hiyo mwenzao hakuwepo na kwamba mama
huyo amekuwa akiwachezea sehemu zao za siri huku akiwapaka mafuta katika
sehemu zao hizo.
Aidha
watoto hao walidai kuwa mara baada ya kuwachezea sehemu zao za siri,
huwa anawashawishi kufanya nao mapenzi kwa zamu huku wengine wakiendelea
kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili wake yakiwemo matiti yake.
“Watoto
hao walidai kuwa, mara baada ya mama huyo kuwachezea, humtaka mmoja wao
kufanya nae mapenzi na hao wengine kumshikashika sehemu mbalimbali za
mwili wake na kwenye maziwa,na baada ya kutimiza haja zake, huwataka
kuondoka mara moja”alisema.
Kamanda
Boaz aliendelea kusema kuwa uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha ya
kuwa mwanamke huyo amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana
mmoja aliekuwa amemaliza darasa la saba miaka mitano iliyopita na
kujaliwa kuzaa nae mtoto mmoja.
Hata
hivyo kamanda huyo alisema kuwa baada ya idara ya utswi wa jamii,kupata
taarifa ya mahusiano hayo, idara hiyo ililifuatilia suala hilo, na
hatimae kukatisha mahusiano yao hayo.
---via gazeti la MAJIRA / na Imma Matukio blog
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako