Jumapili
January 19 kulitokea kifo cha kutatanisha cha mtoto aliyekua akisoma
shule ya msingi Yombo Vituka darasa la pili ambaye alikua anaingia
darasa la tatu mwaka huu Rahma Abeid Karim ambaye taarifa inasemekana
alijinyonga chumbani kwake.
Millardayo.com imefatilia kwa undani taarifa hizi baada ya kuzipata
kwa sababu ya umri mdogo aliokua nao marehemu na pia tulitaka kufahamu
usahihi wa taarifa hizi za kujinyonga ambapo tulipata nafasi ya
kuzungumza na baba wa mzazi wa Rahma Mr.Karim Abeid Kihiyo.
Mr.Kihiyo alianza kuelezea siku ya tukio ilivyokua>>’Ni kifo
cha kusikitisha nakumbuka siku ya Jumapili[Jan 19] nilikuwa chumbani
kwangu,kawaida mwanangu huwa ana tabia ya kuniamsha baba leo huendi
kazini nikamwambia mwanangu naenda,tukanywa chai nae’
‘Baada ya hapo nikaenda Kariakoo nilikua na shughuli za
Kariakoo,ilipofika saa 6 mchana nilipigiwa simu na mke wangu akiwa
analia,akisema mtoto kafa,mtoto kafa nikawa najiuliza nani kafa kwa
sababu hakuna mgonjwa nyumbani,nikampigia simu mpangaji wangu akanambia
mtoto Rahma ni marehemu sasa hivi’
‘Nilikosa nguvu Kariakoo wenzangu walinichukua kwa gari namimi
nilikua na gari yangu kule lakini sikujitambua kama nilikuwa nalo
sikumudu kuendesha hivyo wakanileta nyumbani,kutokea kule mbele ya
barabara yetu hii ya Kigelagela nikaona watu wamejaa nikajua kweli tukio
limetokea’
‘Baada ya kufatilia nikaambiwa mama alikua anafua na mtoto
nje,baadaye mama akamwambia mtoto nenda ndani kanichukulie nguo zako za
shule nikufulie,mtoto akaingia ndani baada ya muda kidogo mama alianza
kumuita,lakini hakuitikiwa akahisi labda mtoto kanyamaza tu’
‘Akaingia ndani aliposhika mlango wa chumbani kwao mlango ulikua
umefungwa,akaona azunguke dirishani akamuona mtoto kajiinamia kitandani
halafu kajifunika nguo,ikiwa juu kajifunika mtandio chini kajifunika
shuka,mama akawa hana wasiwasi pale dirishani aliendelea kuita’
‘Mama alipoona kimya akakimbia ndani akamuita mwanangu mwingine Zena
wakapiga ule mlango bahati nzuri ulifunguka kufika akamkuta mtoto yuko
hoi kitandani akamchukua akamuweka ‘Sebuleni’ wakati huo alikua anahema
kwa mbali sana wakaomba msaada kwa majirani,lakini bahati mbaya
hawakuwahi kufika hospitali kwani alifariki wakiwa njiani.
Marehemu Rahma katikati akiwa na ndugu zake
Msikilize Baba mzazi wa marehemu akielezea tukio hili la kusikitisha kwa kubonyeza play



No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako