WILAYA YA KYELA – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 12.01.2014 MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LEMA NA
KATA YA NGANA, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
BICCO S/O MWAKIBIBI, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LEMA
ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA
WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI
MAWE NA FIMBO. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU NA MWENZAKE
KUVUNJA KIBANDA CHA BIASHARA NA KUIBA, MWENZAKE ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO
HILO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA
UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA
BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKATA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA
HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
WILAYA YA MOMBA – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 12.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:30HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA
SERIKALI WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. ADAMU S/O SILUMBE, MIAKA 27,
MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KAPELE ALIFARIKI DUNIA WAKATI
ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALICHOMWA KISU
MGONGONI TAREHE 10.01.2014 MAJIRA YA SAA 21:00HRS NA MDOGO WAKE AITWAE
BONNY S/O SILUMBE KATIKA KIJIJI CHA KAPELE, KATA YA KAPELE, TARAFA YA
NDALAMBO. CHANZO NI KULIPIZA KISASI BAADA YA MAREHEMU KUMTANGAZA
MTUHUMIWA HAPO KIJIJINI KUWA ALIMTOROSHA MKE WA MTU. MTUHUMIWA ALIKIMBIA
MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU
NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUSHUTUMIANA NA BADALA YAKE WATATUE MIGOGORO YAO
KWA NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUFIKIA MUAFAKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO
HILI AZITOE MARA MOJA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.