Mume wa marehemu Dullah (Tshirt nyeusi mbele ya kamera) akiwasili
makaburini kwa mazishi ya Zainab Buzohera yaliyofanyika leo Jumapili Jan
12, 2014 Tanzania kaika makaburi ya Ukonga, Dar es Salaam, Tanzania
marehemu alizikwa saa 10 jioni kwa saa za Tanzania hapa ilikuwa saa 2
asubuhi (8am ET)
Juu na chini ni Ndugu, jamaa na marafiki wakijiandaa kuutoa mwili wa
mpendwa wetu tayari kwa mazishi yake yalioyofanyika leo Jumapili Jan 12,
2014 Ukonga, Dar es Salaam, Tanzania.
Mwili wa mpendwa wetu ukitolewa kwenye gari lililoubeba kuelekea makaburi ya Ukonga kwa mazishi.
Mosi akisaidia kubeba jeneza lililobeba mwili wa marehemu Zainab
Buzohera mara tu ndugu, jamaa na marafiki walipojumuika na familia
kwenye mazishi ya mpendwa wetu katika makaburi ya Ukonga, Dar leo. Mosi
alishawahiishi DMV miaka ya nyuma.
Kushoto ni baba wa Zainab Mzee Buzo akiwa na ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye maziko ya mpendwa manae
Maziko yakiendelea.
Mume wa marehemu Dullah (Tshirt nyeusi anayefuta mkono na kitambaa) akifuatilia mazishi ya mpendwa mke wake.
kutoka kushoto ni Stephano Mhina, Milanga na Saleh Londa wote walishawahi ishi DMV japo Mhina yupo Tanzania kikazi.
Watatu toka kushoto ni Yassin Njayaga ambaye alishawahi kuwa Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
kwa picha zaidi za mazishi na msiba nyumbani bofya soma zaidi
Umati wa watu waliojumuika pamoja na familia kumzika mpendwa wetu
Zainab Buzohera aliyezikwa leo Jumapili Jan 12, 2014 mida ya saa 10
jioni kwa saa za Tanzania hapa ilikuwa saa 2 asubuhi (8am ET)katika
makaburi ya Ukonga.
Ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani wakiingiza mwili wa
marehemu kwenye gari lililobeba mwili wa mpedwa wetu kuelekea makaburi
ya Ukonga kwa shughli za mazishi yaliyofanyika leo Jumapili Jan 12,
2014. Mwili wa marehemu uliwasili Tanzania siku ya Jumamosi Jan 11,
2014.
Juu na chini gari lililobeba mwili wa Zainab kwa safari yake ya mwisho.
Mama wa Zainab(gauni jeupe kilemba cheusi) akiwa mwenye huzuni huku
akilia kwa uchungu wakati mwili wa Mpendwa mwanae ulipokua ukiingizwa
kwenye gari tayari kwenda kwenye maziko yaliyofanyika leo Jumapili Jan
12, 2014 katika makaburi ya Ukonga mida ya saa 10 jioni kwa saa za
Tanzania hapa ilikuwa saa 2 asubuhi (8am ET).
Wadau kutoka Marekani na wengine ambao waliwahi kuishi Marekani
wakijumuika na familia katika mazishi ya Zainab ambaye amezikwa leo
Jumapili katika makaburi ya Ukonga kwenye picha wa kwanza kushoto ni
Saleh Londa, watatu toka kushoto ni George Mwaswaliba, watano toka
kushoto ni Baraka Kifaru, wasita toka kushoto ni Stephano Mhina, wapili
toka kulia ni Mosi na kulia ni Mussa mkaazi wa New Jersey.
Juu na chini kulia picha juu ni mume wa aliyekuwa Balozi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Shariff Maajar na aliyekaa
kwenye kiti picha chini ni aliyekuwa mwambata wa jeshi Ubalozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali
Maganga wote kwa pamoja wakijumuika na familia kwa maziko ya mpendwa
wetu Zainab Buzohera aliyezikwa leo Jumapili Jan 12, 2014 Tanzania
katika makaburi ya Ukonga.
Msafara wa kuelekea mazikoni
Ndugu, jamaa na marafiki wakielekea mazikoni.